
Wachezaji wa Taifa Stars wakiwasili leo.
Stars iliambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji wao Niger na sasa kukamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi F ambalo lina timu za Uganda “Cranes” pamoja na mabingwa wa Afcon 2019 timu ya Algeria “Desert Foxes” yaani mbweha wa jangwani.
"Tumepata alama 1 ambayo itakuwa ni muhimu kwa siku zijazo lakini tunajiandaa kutafuta alama 3 za nyumbani na tutapambana kupata alama tukiwa uwanjani dhidi ya Algeria”amesema nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta
Stars imeingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo wa pili dhidi ya Algeria utakaofanyika mnamo Juni 8 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam huku timu ya Algeria ikiongoza kundi hilo wakiwa na alama 3 baada ya kuwalaza Uganda kwa kichapo cha mabao 2-0.