Jumatatu , 2nd Jun , 2014

Wadau wa soka wameendelea kuipongeza timu ya taifa ya soka ya Tanzania taifa stars nakulitaka shirikisho la soka nchini TFF kuipeleka kambini haraka badala ya kuanza kusherehekea ushindi huo huku kukiwa na mchezo mgumu mbele

Kikosi cha Stars kikirejea nchini.

Timu ya taifa ya Tanzania taifa stars imerejea nchini jioni ya leo ikitokea nchini Zimbabwe ilikokuwa imekwenda kucheza mchezo wa marudiano wakusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika na kufanikiwa kutinga hatua ya pili ya mtoano baada ya kuiondoa timu ya taifa ya Zimbabwe kwa jumla ya mabao 3-2 , kufuatia sare ya mabao 2-2 huko jijini Harare nchini Zimbwabwe na awali stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Matokeo hayo ya stars ambayo sasa itavaana na msumbiji katika hatua ya pili ya michuano hiyo yamepokelewa kwa shangwe na mashabiki wa soka hapa nchini ambao wamekua wakiipongeza timu hiyo kwa kuonesha mchezo mzuri hapo jana

Mmoja wa wadau wa soka hapa nchini John Jambele pamoja na kuipongeza timu hiyo ametaka maandalizi ya mechi dhidi msumbiji yaanze mapema kwakuwa mchezo unaokuja mbele yao dhidi ya Msumbiji ni mgumu zaidi.