Jumamosi , 13th Nov , 2021

Stephen Curry ameweka rekodi mpya ya kuwa mcheza kikapu pekee mwenye 3-Pointers nyingi kwenye historia ya ligi ya kikapu nchini marekani NBA baada ya kupiga 3-Pointers 9 kwenye mchezo dhidi ya Chicago Bulla alfajiri ya leo.

(Stephen Curry akijaribu kufunga mbele ya walinzi wa Chicago Bulls.)

Curry amefikisha 3-pointers 3, 359 na kuivunja rekodi ya mkongwe wa Milwaukee Bucks, Miami Heat na Boston Celtics, Rey Allen aliyekuwa anashikilia rekodi hiyo kwa muda mrefu akiwa na 3-pointers 3, 358.

3-pointers hizo 9 nimemfanya Curry kujizolea alama 27 na kufikisha alama 40 kwenye mchezo huo zikiwa ni nyingi kuliko mchezaji yeyote, rebound 4 na assist 5 zilizomfanya awe mchezaji bora wa mchezo huo ambao Golden State Warriors wameifunga Chicago Bulls kwa alama  119-93.

Ushindi huo ni wa 10 katika michezo 11 ya NBA msimu huu wa mwaka 2021-22 na kuwafanya Warriors waendelee kuwa vinara wa Western Conference.

NBA itaendelea alfajiri ya kuamkia kesho Novemba 14, 2021 kwa michezo 8, Los Angeles Lakers watacheza dhidi ya San Anonio Spurs saa 5:30 usiku, Utah Jaz dhidi ya Miami Heat saa 7:00 usiku, Cleveland Cavaliers watakipiga na Boston Celtics saa 10:00 alfajiri.