Jumatano , 15th Dec , 2021

Stephen Curry amefunga 3-pointers 6 na kufikisha 2,977 hivyo kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa pekee kwenye historia ya Ligi ya kikapu Marekani ‘NBA’ kuwa na 3-pointers nyingi zaidi na kumpiku gwiji wa zamani wa Milwaukee Bucks, Rey Allen aliyekuwa anaishikilia rekodi hiyo akiwa na 2,973.

(Stephen Curry akijaribu kufunga mbele ya mlinzi wa LA Clippers)

Curry ameweka rekodi hiyo alfajiri ya leo na kuisaidia timu yake ya Golden State Warriors kupata ushindi wa alama 105-96 dhidi ya New York Knicks ambapo pia alifunga alama 22, rebound 3 na Assist 3 na Warriors kurejea kileleni mwa ligi hiyo kwa ukanda wa Magharibi.

(Gwiji Rey Allen (kushoto) akiwa na Curry na Miller ambao walishuhudia Curry akivunja rekodi hiyo)

Curry amevunja rekodi hiyo mbelel ya Rey Allen ambaye alikwepo uwanjani kushuhudia mchezo huo huku wakiwa wenye furaha kubwa na kiwango cha Curry. Curry mwenye miaka 33 kwa sasa bado ana muda wa kuendelea kucheza mchezo huo na kama akifanikiwa kufikisha 3-pointer 23 basi atafikisha 3,000 ambapo ataweka rekodi ya kipekee zaidi kuwa mcheza kikapu wa kwanza kufikisha 3-pointers 3,000.