Alhamisi , 6th Mar , 2014

Timu ya soka ya Taifa Stars kutua nchini kesho mchana

Timu ya soka ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inataraji kurejea nchini kesho mchana ikitokea jijini Windhock Namibia ambako jana usiku ilicheza na wenyeji wao Namibia Brave Warrious na kutoka sare ya bao 1-1.

Afisa Habari wa TFF Boniface Wambura amesema kuwa japokuwa matokeo hayo ya Stars si mabaya, hilo halikuwa lengo la TFF katika safari ya kuhakikisha timu hiyo inapanda katika orodha ya viwango vya FIFA.

Aidha Wambura amesema kuwa lengo lao lilikua ni kuhakikisha timu hiyo inashinda ugenini na kupata point nyingi, lakini kwa matokeo hayo ni wazi stars haitapata point nyingi kwakua Namibia katika viwango vya ubora vya FIFA iko chini yetu.