Tanzania imefanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kuitwanga Comoros kwa mabao 2-1 siku ya jana Novemba 18.
Vijana wa Boniface Pawasa wakifanikiwa kufuzu fainali ya michuano hii watashuka uwanjani siku ya Jumamosi kuwania taji hilo.
Huu ni muendelezo wa timu ya taifa ya ufukweni kwenye kufanya vizuri kwa mashindano ya kimataifa baada ya kufanikiwa kufuzu mashindano ya AFCON mwaka huu licha ya kushindwa kushiriki kutokana na kushindwa kufika baada ya kukosa fedha za usafiri.