
Mcheza kikapu chipukizi aliyefariki Dunia mchana wa jana, Terrence Clarke.
Clarke aliyefariki akiwa na umri wa miaka 19, mwenye urefu wa futi 6 na inchi 7 alikuwa anatajwa kuwa miongoni mwa wacheza kikapu bora chipukizi tena kutoka kwenye nafasi ya ulinzi tokea mwaka 2020 jambo ambalo limewagusa mashabiki wengi wa mchezo huo Duniani.
Baada ya kifo hiko kutangazwa, aliyekuwa kocha wake, John Calipari amesema; “Wote tupo kwenye mshangao mkubwa. Hiki kitakuwa kipindi kigumu kwa wote waliomfahamu na kumpenda Terrence, na nimuombe kila mmoja achukue wasaa usiku wa leo kumuombea Terrence na familia yake. Apumzike kwa amani”.
Terrence ambaye alikuwa na ndoto ya kucheza NBA, mwezi uliopita alisaini mkataba wa kuendelea kucheza ligi hiyo ambapo aliambulia kucheza michezo 8 tu ya msimu uliopita baada ya kusumbuliwa na majeraha kwenye mguu wake wa kulia.