Jumatano , 18th Mar , 2015

Bodi ya Ligi Tanzania TPBL imesema imeweza kukutana na Uongozi wa TFF na kujadili juu ya mabadiliko ya Ratiba yaliyokuwa yakijitokeza katika michuano ya Ligi kuu Soka Tanzania Bara.

Akizungumza na East Africa Radio, Kaimu Ofisa Mtendaji wa TPLB, Fatma Abdallah amesema baada ya kukutana waliweza kujadili na kufanya marekebisho ya ratiba ambayo hayatokuwa tena na mabadiliko yoyote kwa timu zote shiriki za Ligi kuu Soka Tanzania Bara mpaka Ligi itakapomalizika.

Fatma amesema, ratiba kamili ya Ligi inayoendelea hivi sasa ni ileile ya hapo awali lakini wamefanya marekebisho kidogo ili kuweza kuzuia mabadiliko hayo.

Fatma amesema, vilabu vilipokuwa vikilalamika juu ya mabadiliko hayo vilikuwa sawa kwani walikuwa wakikaa na kujadili lakini taarifa zilikuwa zikichelewa kuwafikia.