Jumatatu , 25th Jan , 2016

Chama cha Mpira wa Magongo nchini THA kimesema kipo kwenye taratibu za awali za maandalizi ya Ratiba ya Ligi ya Klabu bingwa Mkoa wa Dar es salaam.

Katibu wa THA Mnonda Magani amesema, wapo katika utaratibu wa kuandaa ratiba ili kuepusha kuingiliana na kalenda ya Shirikisho la Mchezo huo Afrika AHF.

Magani amesema, wamechelewa kujua muda na mahali watakapochezea ligi hiyo kutokana na kuchelewa kwa kalenda ya AHF ambayo inaandaa Michuano ya Bingwa Afrika.

Magani amesema, ratiba hizo zimeingiliana kutokana na ushiriki wa Tanznaia katika Ligi ya Klabu bingwa Afrika ambayo nao wapo katika maandalizi ya awali.

Magani amesema, Tanzania inawakilishwa na timu ya TPDF kwa upande wa wanaume na Tanzania Twende kwa upande wa wanawake ambao ndio waliibuka na Ubingwa katika mashindano ya Klabu bingwa ya Magongo.