
Nembo ya ligi kuu soka Tanzania bara
Tayari timu moja imeshashuka daraja ambayo ni African Lyon yenye pointi 23 baada ya mechi 37, huku timu nyingine nane kuanzia nafasi ya 12 hadi ya 19, zikiwa na tofauti ya pointi 1 hadi 3 hivyo kufanya kila timu iwe na nafasi ya kushuka au kubaki ligi kuu leo.
Kundi la kwanza kwenye timu 8 zilizopo kwenye hatari ya kushuka ni Biashara United, JKT Tanzania, Stand United na Mbao FC zenye pointi 44 katika nafasi ya 12 hadi 15. Tofauti ya hizi timu ni idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa.
Kundi la pili ni timu za Tanzania Prison na Kagera Sugar ambazo zipo katika nafasi ya 16 na 17 zikitofautiana idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa.
Kundi la mwisho ambalo lipo kwenye hatari zaidi ni Ruvu Shooting yenye pointi 42 katika nafasi ya 18 na Mwadui FC yenye pointi 41 katika nafasi ya 19. Zenyewe zinahitaji matokeo ya ushindi tu huku pia zikisubiri matokeo ya wengine waliopo juu yao.
Jumla ya mechi 10 kupigwa leo.
Ratiba michezo ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara. pic.twitter.com/nPI4tf0uzq
— TFF TANZANIA (@Tanfootball) May 28, 2019