Katika michezo ya mwisho ya kundi B iliyokamilika jioni hii imeshuhudiwa pia timu ya JKT Tanzania ambayo imeshafuzu ikimaliza kileleni mwa kundi hilo kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mshikamano.
Msimu ujao jumla ya timu sita zitakuwa mpya kwenye ligi huku timu mbili zikishuka daraja kutoka kwenye timu 16 zilizoshiriki ligi msimu huu. Msimu ujao pia jumla ya timu 20 zitacheza ligi kuu.
Timu zingine zilizopanda daraja msimu huu ni Biashara Mara, Alliance Schools ya Mwanza, Coastal Union ya Tanga, JKT Tanzania ya P wani na KMC ya Dar es salaam.





