Jumanne , 18th Jul , 2017

Ikiwa imebakia siku chache vumbi kutimuka katika michuano ya mpira wa kikapu ya Sprite BBall Kings hatua ya nusu fainali timu ya TMT imeanza majigambo yake na kudai itaendeleza kutoa kichapo kwa wapinzani wao watakaokutana nao siku ya Jumamosi

Kikosi cha timu ya TMT.

katika uwanja wa Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya nahodha wa timu yake, Salim Mohamed Mustapha amesema katika hatua hii ya nusu fainali ya michuano ya mpira wa kikapu ya Sprite BBall Kings wataendelea kushirikiana kwa pamoja kama timu ili waweze kufika hatua ya fainali.

"Tutaendelea kucheza game yetu ile ile ambayo imetufikisha mpaka hapa tulipofika kwa sababu ukiangalia kwenye 'statistics' za wachezaji 'individual' utaona wachezaji wetu wengi hawapo katika hizo statistics lakini mechi zetu sisi tumeshinda kwa pointi 20, 50, 23 kwa hiyo inamaanisha sisi tunacheza kitimu zaidi kuliko kibinafsi, tunaendelea kucheza na moto huo huo na mwisho wa siku utatufikisha fainali na kushinda kabisa kitita cha Milioni 10", amesema Mustapha.

Timu ya TMT ilipata nafasi ya kuingia hatua hiyo baada ya kumchakaza mpinzani wake Dream Cheaser kwa pointi 73-96 sawa na tofauti ya pointi 23 mchezo uliyochezwa katika viwanja vya chuo kikuu (UDSM) Jijini Dar es Salaam.