
(Kocha wa Simba, Pablo Franco (kushoto) na Mohammed Bares wa JKT TZ)
Bares amesema, "JKT Tanzania tumechezabna Simba mara nyingi kwa hiyo sioni kitu kigeni, tunawajua, tumepanga kuwashangaza watu kwa kuwatoa mabingwa watetezi mapema kwenye michuano ya mwaka huu na siyo kuwakamia bali uwezo tulionao"
Lakini baada ya tambo hizo, Bares alisisitiza kuwaheshimu Simba kwasababu wana wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kuamua matokeo wawapo uwanjani.
"Tunawaheshimu sana Simba, tunaenda kucheza nao kwa tahadhari kubwa kwa sababu wapinzania wetu ni imara na wachezaji wake wanauwezo wa kutafuta matokeo katika kipindi chote cha dakika 90" Amesema Bares.
Kwa Upande wa mabingwa watetezi wa Kombe hilo, Kocha wake Pablo Franco Martin amesema anafikiria ushindi tu na si vinginevyo kutokana na umuhimu wa ushindi huo na kutamba inawezakan kuupata kwani wachezaji wake wanajitambua.
"Mechi ni muhimu sana kushinda. Tumejiandaa vizuri wachezaji morali ipo juu. Kila mmoja anatambua majukumu yake kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania" Amesema Pablo.