Jumatano , 29th Sep , 2021

Timu ya taifa ya soka ya Wanawake Tanzania ‘Twiga Stars’ inataraji kuanza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi michuano ya kanda za nchi za kusini mwa Afrika COSAFA saa 9:30 Alasiri ya leo Septemba 29, 2021 dhidi ya Zimbabwe kwenye uwanja wa Nelson mandela Bay nchini Afrika kusini.

Kocha wa Twiga Stars, Bakari Shime akitoa maelekezo kwa wachezaji wake akiwa benchini.

Kuelekea kwenye mchezo huo, Kocha wa Twiga Stars, Bakari Shime amesema wachezaji wapo vizuri na wamejiandaa vizuri na mchezo huo ukizingatia wanagahamu vizuri wapinzani wao.

"Namshukuru Mungu tupo salama, tumefanya maandalizi leo na wachezaji wana ari kubwa ya mchezo huo" Alisema Shime.

Twiga Stars ipo kundi B na timu za Zimbabwe, Botswana na Sudan kusini huku ikitaraji kushuka tena dimbani Oktoba 2, 2021 kucheza na Botswana kabla ya kucheza na Sudan Kusini.