Ubingwa wa FA kumbakisha Aubameyang Arsenal?

Ijumaa , 31st Jul , 2020

Kocha wa klabu ya Arsenal ,Mikel Arteta amesema iwapo timu yake itafanikiwa kutwaa ubingwa wa FA itamshawishi mshambuliaji Pierre -Emerick Aubameyang kusalia klabuni hapo.

Mshambuliaji wa Arsenal, Piere-Emerick Aubameyang katika majukumu ayke uwanjani.

 

Kauli hiyo ameitoa wakati Arsenal inajiandaa kuikabili Chelsea katika fainali itakayopigwa kesho kwenye dimba la Wembley ambapo The Gunners itahitaji kushinda ili ijihakikishie nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao.

Arteta amesema kuwa kushinda taji kunaongeza kujiamini na hivyo iwapo watafanya hivyo kutamshawishi Aubameyang kusaini mkataba wa kuendelea kubaki Emirate kwa miaka mingine zaidi kwani wa sasa utamalizika mwakani.

Arsenal ilimaliza nafasi ya 8 katika EPL, hivyo haina nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya moja kwa moja .