Ijumaa , 11th Jan , 2019

Shirikisho la soka nchini (TFF), kupitia kwa Mwenyekiti wake wa Kamati ya Uchaguzi, Malangwe Mchungahela, limeweka wazi kuwa limepokea maelekezo ya mahakama kuwa uchaguzi wa Yanga umepingwa na wanachama wa klabu.

Makao makuu ya Yanga

Akiongea leo jijini Dar es salaam, Malangwe Mchungahela amesema leo wakiwa kwenye kikao cha maandalizi ya uchaguzi na viongozi wa Yanga wamepokea taarifa ya wanachama wa Yanga katika mikoa mbalimbali kufungua kesi ya kupinga uchaguzi.

''Uchaguzi wa Yanga uliopangwa kufanyika Januari 13, 2019 umesimamishwa baada ya wanachama wa Yanga katika mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Morogoro na maeneo mengine kufungua kesi mahakamani kupinga uchaguzi huo'', amesema.

Aidha Mchungahela amesema kutokana na umuhimu wa muhimili huo, hawawezi kupingana nao hivyo shughuli zote ikiwemo kampeni zimesimamishwa mpaka pale maelekezo mengine yatakapotolewa.

Yanga ilikuwa inangia kwenye uchaguzi huo ili kuziba nafasi za viongozi zilizoachwa wazi baada ya wengi wao kujiuzulu.

WAGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI

Dk. Jonas Tiboroha, Mbaraka Hussein Igangula na Erick Ninga.

MAKAMU MWENYEKITI
Yono Kevela, Titus Osoro, Salum Magege

WAJUMBE KAMATI YA UTENDAJI NAFASI 4
Hamad Islam, Benjamin Mwakasonda, Sylvestre Haule, Salim Seif, Shafil Amri, Said Kambi, Dominick Francis, Seko Jihadhari, Ally Omar Msigwa, Arafat Ally Hajji, Frank Kalokola, Ramadhani Said, Leonard Marango, Bernard Faustin Mabula, Christopher Kashiririka na Athanas Peter Kazige.

WALIOJIUZULU

Mwenyekiti: Yussuf Manji,
Makamu Mwenyekiti: Clement Sanga
Wajumbe wanne: Omary Said Amir, Salum Mkemi, Ayoub Nyenzi na Hashim Abdallah.