Ijumaa , 23rd Jul , 2021

Julai 25, 2021 ambayo ni siku ya Jumapili itakuwa ni Fainali ya Azam Sports Federation (ASF) ikuwakutanisha miamba wawili wa kabumbu nchini klabu ya Simba na Yanga huku ikiwa ndio fainali ya kwanza ya ASF kukutana.

Picha ya Mchezaji Shomari Kapombe na Ditram Nchimbi

Siku zote Fainali huwa ni ngumu lakini hii kuna mambo matatu ambayo yanaifanya kuwa ngumu zaidi ambayo ni;

1.Upinzani wa Jadi (Derby) uliopo kati ya vilabu hivi vikubwa vya soka nchini Tanzania kwani vimekuwa kwenye hali hiyo ya upinzani mkubwa kwa miaka mingi.

2.Kumbukumbu ya matokeo mabaya ya hivi karibuni kwa klabu ya Simba dhidi ya mpinzani wake Yanga, kwani atataka kudhihirisha ubora wake baada ya msimu huu kupoteza mchezo Julai 3 kwa goli moja na kutoka sare ya kufungana goli 1.

3.Yanga kutaka kuendeleza ubabe dhidi ya Simba na kutwaa kombe kubwa la kwanza baada ya misimu mitatu kupita mbele ya bingwa mtetezi na kutimiza ile ahadi ya kutwaa vikombe msimu wa 2020/21.