Jumatano , 20th Mei , 2020

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Klabu ya Simba SC, imetangaza kufanya jambo kubwa na la kihistoria siku ya Jumamosi Mei 23, 2020 ifikapo saa 7:00 mchana.

Picha ya kikosi cha Simba SC 2019/2020

Simba SC imetangaza jambo hilo kupitia katika ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo wameandika,

"Unaikumbuka saa 7 mchana, tukutane Jumamosi hii Mei 23, 2020. Historia mpya kwa klabu kaa tayari NguvuMoja"

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Historia mpya kwa klabu. Kaa tayari. #NguvuMoja

A post shared by Simba Sports Club (@simbasctanzania) on

Sasa kama unaikumbuka Saa 7 Mchana ilikuwa ni sera mpya ya Simba SC, ambapo walikuwa wanatumia wakati huo kutambulisha na kuwasaini wachezaji wao wapya, matukio makubwa au jambo lolote lililohusu klabu hiyo.