Alhamisi , 9th Sep , 2021

Mwanariadha mwenye kasi zaidi Ulimwenguni, Usain Bolt, 35, amesema kuwa ni mapema sana kwasasa kurejea kwenye hali ya ushindani baada ya kupata majereha, ingawa ameweka wazi kuwa anashauku kubwa kurejea uwanjani.

Usain Bolt.

Mjamaika huyo ametanabaisha alikuwa mbioni kurejea katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika Tokyo, Japan mwaka huu ila kocha wake alimshauri asiharakishe urejeo wake.

Bolt ambaye ni mshindi mara nane kwenye mashindano ya Olimpiki ameongeza kuwa alikuwa na mpango wa kustaafu riadha, ingawa Kocha wake alimwambia kuwa ahakikishe anauhakika na uamuzi wake kwasababu hatokuwa tayari kufanya nae kazi kwa mara ya pili iwapo atajiondoa katika ushindani.

Nyota huyo pia anaamini upinzani kati ya wanariadha wa kike wa Jamaika, Shelly-Ann Fraser Pryce na Elaine Thompson-Herah inaweza kusababisha mmoja wao kuvunja rekodi za ulimwengu za 100m na 200m, zilizowekwa na Mmarekani Florence Griffith Joyner mnamo 1988.