Jumatano , 3rd Jun , 2015

Viongozi wa soka nchini wametakiwa kujitahidi, kujitambua na kuwa makini katika suala zima la kuwandaa vijana wenye vipaji vya soka ili kuweza kukuza soka hapa nchini.

Jezi mpya za Taifa Stars zilizozinduliwa leo kutoka kushoto ni Jezi ya mazoezi, Jezi ya nyumbani na jezi ya ugenini

Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya shirikisho la Soka nchini TFF Tangu kujiunga na Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulimwenguni FIFA iliyoambatana na zoezi la uzinduzi wa jezi mpya za Timu ya Taifa taifa Stars pamoja na ugawaji wa vyeti kwa waliochangia ukuaji wa soka nchini, Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Mpira wa miguu FAT Alhaj Muhidin Ahmad Ndolanga amesema, vijana wengi wanavipaji lakini haviendelezwi.

Ndolanga amesema, vijana wengi wana vipaji vya soka na vipaji havifufuliwi bali vinatakiwa kuendelezwa kutokana na vijana hao kuzaliwa wakiwa na vipaji vya soka ambavyo vinatakiwa kukuzwa ili kupata vipaji vingi.

Ndolanga amesema, iwapo vipaji vya vijana hao vikiendelezwa itasaidia kupata vijana watakaofanya vizuri katika mashindano mbalimbali na kuweza kuitangaza nchi katika ramani ya michezo.