Jumamosi , 31st Mei , 2014

Viwango na ubora ukiambatana na uwezo wa vipaji binafsi vya wanamichezo wa michezo mbalimbali wanaoshiriki michuano ya shule za sekondari mkoa wa Dar es salaam vyafanya viongozi wao kutamba kuibuka washindi wa jumla michuano ya taifa

Wanamichezo mbalimbali wakiandamana wakati wa ufunguzi wa mashindano ya UMISETA Dar es salaam

Uongozi wa Kamati ya mashindano yanayoshirikisha Shule za Sekondari ya UMISETA kanda ya Dar es salaam, umesema unatarajia kupata timu bora itakayoiwakilisha kanda hiyo katika michuano ya UMISETA taifa itakayofanyika Kibaha Mkoani Pwani.

Akiongea na Muhtasari wa Michezo,Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Omath Sanga amesema wachezaji wa michezo mbalimbali kutoka mikoa mitatu ya Ilala, Temeke na Kinondoni wamekuwa wakionesha vipaji vya hali ya juu katika michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Soka, Netibali na Riadha

Aidha Sanga amesema kwa hali ilivyo sasa wanategemea kikosi cha mkoa wa Dar es salaam kitakachoundwa na nyota wa michezo mbalimbali kutoka katika mashindano hayo yanayoshirikisha mikoa ya kimichezo ya Ilala, Kinondoni na Temeke kitakuwa ni kikosi bora sana kuliko misimu iliyopita na wana matumaini ya kutwaa ubingwa wa jumla kama ilivyokuwa misimu miwili iliyopita.