Vita ya Manara na Jerry Muro yarejea tena

Jumapili , 9th Feb , 2020

Ile vita ya maneno iliyokuwa ikivuma miaka takribani mine iliyopita kati ya Afisa Habari wa Simba, Haji Manara na Aliyekuwa Afisa Habari wa Yanga, ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro imerejea tena.

Haji Manara na Jerry Muro

Hiyo imejidhihirisha katika ukurasa wa kijamii wa Instagram wa Haji Manara, baada ya kuposti picha inayoonesha data ya listi ya klabu zilizofanya vizuri barani Afrika katika mtandao wa Facebook kwa mwezi Januari 2020.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Morning Guys 

A post shared by Haji S. Manara (@hajismanara) on

Baaada ya kuposti picha hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ambaye ni shabiki kindakindaki wa Yanga alikuja na kuweka maoni yake, akisema kuwa Simba hivi sasa inajikita na data za Facebook badala ya kucheza na kupata matokeo mazuri uwanjani.

"Ndugu yangu jifunze Kiingereza kidogo uelewe, kwahiyo siku hizi Simba kazi yake ni kucheza mpira Facebook na sio uwanjani?. Aibu gani hii, sisi tulidhani ni viwango vya ubora uwanjani kumbe viwango vya Facebook, kweli haya maajabu unayapata Simba tu", ameandika Jerry Muro katika maoni yake.

"Heri ya Yanga yeye anapiga mpira na kushinda uwanjani sio Facebook akili ya Haji Manara anaijua mwenyewe", ameongeza.

Yanga imeendelea kufanya vizuri katika mechi za hivi karibuni, ikishinda mechi nne mfululizo za ligi na kufikisha pointi 37 katika nafasi ya tatu, huku Simba ikishinda mechi tano za karibuni na kupoteza mechi moja na kufikisha pointi 50 katika nafasi ya kwanza.