Wachezaji wa Yanga
Mchezo wa mapema unachezwa majira ya Saa 8 mchana. Mwadui FC ambao wameshashuka daraja watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar wanao shika nafasi ya 13 kwenye ligi wakiwa na alama 34, mchezo huu unachezwa katika dimba la Mwadui Complex huko mkoani shinyanga.
Saa 10:00 Jioni Dodoma Jiji watakuwa wenyeji wa KMC ya Dar es salaam katika Dimba la Jamuhuri. Timu hizi zinatofautiana alama 2 tu kwenye msimamo, KMC wapo juu wakiwa nafasi ya 6 na alama zao 41 wakati Dodoma wana alama 39 wakiwa nafasi ya 9. Mchezo wa mkondo wa kwanza KMC ilishinda kwa bao 1-0.
Na Mchezo wa Mwisho kesho Ruvu shooting watakuwa wenyeji wa Yanga SC majira ya Saa 1:00 Usiku. Ruvu shooting watakuwa na kibarua cha kufuta uteja mbele ya Yanga, kwani kwenye michezo 8 ya mwisho kukutana wameshinda mara moja tu, na mchezo wa mkondo wa kwanza msimu huu walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.
Ruvu shooting wapo nafasi ya 10 na alama 37, wakati Yanga wana alama 61 wakiwa wanamili nafasi ya pili.