Wababe wa Simba wapelekwa Mbeya

Alhamisi , 10th Jan , 2019

Klabu ya soka ya Mashujaa FC kutoka Kigoma imepangwa kucheza na Mbeya City ya jijini Mbeya katika mzunguko wa nne na wa tano wa michuano ya Kombe la shirikisho Tanzania.

Shiza Kichuya akiwania mpira na moja ya wachezaji wa Mashujaa FC.

Katika droo iliyofanyika leo jijini Dar es salaam Mashujaa FC ambao waliowaondoa Simba katika mzunguko wa tatu kwa kipigo cha mabao 3-2 watasafiri kwenda kucheza kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Kwa upande mwingine klabu ya Azam FC imepangwa kucheza na Pamba FC ya Mwanza katika mchezo ambao utapigwa kwenye uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es salaam.

Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Mtibwa Sugar watacheza na Majimaji FC kwenye uwanja wa Manungu Turiani Morogoro.

Mabingwa wa msimu wa 2015/16 klabu ya Yanga watakipiga na..... kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Michezo hiyo ya mzunguko wa nne itafanyika kati ya tarehe 25 na 28 mwezi Januari, 2019. Mchezo wa fainali mwaka huu utapigwa kwenye uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.