Alhamisi , 12th Mei , 2016

Wadau wameombwa kutoa msaada wa vifaa kwa mabondia ili kuweza kuwa na maandalizi mazuri kabla ya kwenda kwenye mashindano ya ridhaa ya Kimataifa.

Wadau wameombwa kutoa msaada wa vifaa kwa mabondia ili kuweza kuwa na maandalizi mazuri kabla ya kwenda kwenye mashindano ya ridhaa ya Kimataifa.

Rais wa Shirikisho la Masumbwi Tanzania (BFT) Muta Rwakatare, amesema timu ya taifa ya masumbwi ilifanya vibaya kwenye michuano ya Jumuiya ya Madola ya mwaka 2014 nchini Scotland, kwa kukosa baadhi ya vifaa kama viatu na gloves.

Rwakatare ametoa ombi hilo baada ya hivi karibuni Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kukabidhi ulingo wa ngumi kwa Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ, ambapo ametaka vifaa vingine vitolewe kwa mabondia kusaidia maandalizi.