Jumamosi , 31st Mei , 2014

Sholinj Camp wakishirikiana na wanamichezo wengine wa sanaa ya mapigano wafanya tamasha kubwa la kumbukumbu ya mwanzilishi wa Sholinj Camp jijini Dar es salaam Tanzania

Wanamichezo wa sanaa ya mapigano wakiwa katika picha ya pamoja katika moja ya maonesho yao.

Wanamichezo mbalimbali wa aina tofauti za michezo ya sanaa ya mapigano jijini Dar es salaam wamekutana hii leo katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es salaam katika Kuadhimisha kumbukumbu ya mwanzilishi wa mchezo wa sholinj Camp Kaiso Doshing Sol

Mratibu wa tamasha hilo lijulikanalo kama Kaiso day 'Shokensh' Tedson Elam toka Sholinj camp amesema wamewaalika pia wenzao kutoka katika michezo ya shotokan karate, shaolin kun fu na tai chi ili kubadilishana uzoefu kutokana na michezo hiyo kuonekana kufanana lakini.

Kwa upande wake mmoja wa walimu wa sanaa ya mapigano Jafar Bashiri amesema mchezo wa sholinj camp, Masho Arts ni sanaa ya mapigano ambayo iko katika kuijenga jamii yenye misingi bora ya kuishi katika jamii ambayo ina maadili bora.

Naye mmoja wa wakufunzi wa Shotokan Karate Sensei Phillip Chikoko amesema kualikwa kwao katika tamasha hilo la kumbukumbu wa siku hiyo ya muanzilinzi wa Shalinji Camp kunasaidia kuimarisha uhusiano wa wanamichezo wa sanaa hizo za mapigano.