Jumatano , 25th Feb , 2015

Wanariadha sita kutoka Tanzania wanatarajia kuingia kambini mwezi huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mbio za Dunia yanayotarajiwa kufanyika Machi 28 mwaka huu nchini China.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha nchini RT, Suleiman Nyambui amesema, katika mashindano hayo yatakayoshirikisha nchi mbalimbali duniani, yanahitaji kuwa na washiriki watatu kutoka kila nchi ambapo watatu wengine ni akiba iwapo kunatatizo litatokea.

Nyambui amesema, Shirikisho la Riadha la kimataifa IAAF limehakikisha linagharamikia nchi shiriki ili kuhakikisha nchi hizo zinashiriki kikamilifu na kuweza kushinda mashindano hayo.