Watatu wa Kimataifa kuikosa Yanga leo

Jumapili , 6th Oct , 2019

Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara VPL kati ya Yanga na Coastal Union leo, jumla ya wachezaji watatu wa Kimataifa wa Yanga watakosekana leo kwenye mchezo huo.

Baadhi ya wachezaji wa kigeni wa Yanga

Akizungumzia juu ya majeraha ya klabu hiyo, Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa licha ya kuwakosa wachezaji hao, timu yao inatambua kuwa ina mzigo mkubwa kutokana na matokeo mabovu waliyoyapata hivyo watafanya vizuri kutokana na wachezaji walio nao.

"Tunawakosa wachezaji kama Lamine Moro, Patrick Sibomana na Sergi pamoja na kiungo Mtanzania, Mohamed Banka, tumepoteza mechi ya kwanza na tumetoa sare mechi ya pili hivyo wale watakaopangwa watacheza vizuri", amesema Hafidh.

Mchezo wa leo ni wa tatu kwa Yanga katika ligi, ambapo mpaka sasa ina pointi moja tu baada ya kupoteza mechi ya kwanza dhidi ya Ruvu Shooting na kutoka sare katika mechi ya pili dhidi ya Polisi Tanzania.