Jumatano , 15th Mei , 2019

Baada ya hivi karibuni kuwepo kwa tetesi kuwa mabingwa wa soka nchini England klabu ya Manchester City, huenda wakakutana na kifungo cha kutoshiriki Ligi ya Mabingwa.

Manchester City

Suala ya Man City kufungiwa, lipo chini ya wachunguzi wa Uefa ambao wanataka klabu hiyo ipigwe marufuku kushiriki UEFA kwa msimu mmoja iwapo watapatikana na hatia ya kuvunja sheria ya kifedha. 

Licha ya kuwa chini ya wachunguzi hao lakini maamuzi ya mwisho yapo chini ya mchunguzi mkuu Yves Leterme. 

Yves Leterme ni Waziri mkuu wa zamani wa Ubelgiji, ambaye alihudumu kutoka March 2018 hadi Desemba 2018. Na ndio mwenyekiti wa jopo la wachunguzi wa shirikisho la soka la Uefa.

Jopo hilo linatarajiwa kufanya maamuzi ndani ya wiki hii lakini maamuzi ya mwisho yanabaki kuwa chini yake hivyo anaweza kupendekeza wafungiwe ama vinginevyo.

Hata hivyo imeelezwa katika mkutano wa hivi karibuni wenzake wanaaaminika kutoa msimamo wao kwamba marufuku ya msimu mmoja kwa mabingwa hao inatosha.