Jumatano , 24th Feb , 2016

Kocha mkuu wa Arsenal Arsene Wenger amesema Barcelona imefuzu asilimia 95 katika michuano ya robo fainali ya kombe la vilabu bingwa barani Ulaya, baada ya kilabu yake kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Barcelona usiku wa jana kwenye uwanja wa Emirates.

Mfaransa huyo amelaumu safu yake ya mashambulizi kwa kushindwa kufunga na kukosa kujua cha kufanya wakati wa mechi hiyo.

Alex Oxlaide Chamberlain na Olivier Giroud walikosa nafasi za wazi kwa upande wa Arsenal kabla ya Barcelona kufunga bao lao la kwanza.

''Vile tulivyomaliza nafasi zetu ilikuwa matatizo.Nilihisi katika kipindi cha mwisho tulikosa kufanya kitu muhimu,'' alisema Wenger.

Wenger amesema Barcelona kimahesabu wameshafuzu, lakini vijana wake watakwenda kupambana tena kwenye mechi ya marudiano na si kwenda kuchezeshwa.