
Eddie Hearn ambaye ni promota mashughuli wa mchezo wa masumbwi Duniani.
Kushindikana kwa mapatano mawili ya kupambana kati ya Anthony Joshua na Tyson Fury yatamaanisha kwamba Deontay Wilder hatapokea taji la ulimwengu kwa zaidi ya mwaka mmoja, anasema promota Eddie Hearn.
Bingwa wa WBC Fury alitangaza mwezi huu kwamba hana mpango wa kupigana na Wilder baada ya kushindwa kukubaliana na badala yake atatafuta pambano la kurudi nyumbani mnamo Desemba.
Kwa upande wa Antony Joshua anarudi mwezi huo huo, akitetea mikanda yake ya WBA, IBF na WBO dhidi ya Kubrat Pulev mnamo Desemba 12.