Ijumaa , 23rd Apr , 2021

Kuelekea kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Azam utakaochezwa Jumapili ya April 23, 2021, majira ya saa mbili usiku, mchezaji wa zamani wa Azam, Saidi Moladi amesemea wachezaji wa Azam wanapaswa kuepuka presha na kujitambua ili wapate ushindi.

Saidi Moladi

Akizungumza na Eatv saa moja michezo mchezaji huyo amesema katika kipindi ambacho alikuwa anacheza akiwa chini ya kocha Sterwart Hall walikuwa wanawaelekezwa kucheza kwa kuiheshimu Yanga tena bila kubweteka kwasababu Yanga inafungika.

''kama Azam inataka ushindi katika mechi hiyo wachezaji wahamasishane na kila mchezaji awe askari wa mwenzie, na kuacha kucheza kwa ubinafsi wacheze kitimu naamini wanaweza kupata matokeo '' amesema Said Moladi.

Kwa upande mwingine mchezaji huyo amesema yupo tayari kurejea katika ligi kuu endapo timu yoyote ikihitaji huduma yake.

'' kwasasa sina timu ila nimeitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya soka la ufukweni ambapo tunajiandaa na michuano ya BSAFCON 2021 yatakayofanyika Senegal mwenzi mei'' amesema Said Moladi.