Kikosi cha Yanga
Kesho Jumapili, African Lyon inatarajiwa kucheza na Simba kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Mbao FC itakuwa mwenyeji wa Azam FC Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kwa upande wake, Ndanda itakuwa mwenyeji wa Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati Tanzania Prisons inatarajiwa kuialika Young Africans kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Kagera Sugar kwa upande wake Jumapili itacheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, ilihali JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Toto Africans kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
Ligi hiyo itaendelea Jumatatu kwa michezo miwili ambako Mtibwa Sugar itaialika Mbeya City kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Morogoro wakati Mwadui itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Mwadui ulioko Shinyanga