Ijumaa , 18th Mei , 2018

Watani hao wajadi kutoka Tanzania Simba na Yanga  wataungana na wenzao Singida FC na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ya Zanzibar katika michuano ya kuwania Kombe la Sports Pesa.

Gor Mahia ni miongoni mwa timu nne za Kenya zitakazoshiriki pamoja na watani wao wa jadi AFC Leopards, Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboyz ambapo jumla ya dola 57,500 zitashindaniwa katika mashindano hayo ya wiki moja yatakayofanyika kwenye Uwanja wa Kasarani.

Afisa mkuu wa mauzo ya kampuni ya mchezo wa kubahatisha SportPesa, Kelvin Twissa, amesema mashindano hayo yatazidi kuboresha uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Kenya.

“Tumechagua timu bora zilizonawiri katika ligi zao kuu za nyumbani mwaka jana, na pia hii ni njia moja ya kukuuza vipaji vya kandanda eneo letu,'' alisema Twissa.

Mshindi wa mashindano hayo atasafiri hadi England kutoana jasho na Everton katika uwanja wao wa Goodson Park mwezi wa saba.