Jumapili , 25th Feb , 2018

Klabu ya soka ya Yanga kupitia msemaji wake Dismas Ten imefunguka na kudai hakukuwa na taarifa zozote zilizotolewa kuwa kiungo wao Thabani Kamusoko ataweza kurudi dimbani bali taarifa iliyotolewa ni ya kupona majeraha aliyekuwa nayo.

Dismas ametoa ufafanuzi huo baada ya Kamusoko kutoonekana uwanjani katika mechi mbili zilizopita ikiwa pamoja na kutokuwepo katika msafara wa wachezaji waliokwenda katika visiwa vya Sheli Sheli kwenye mchezo wa klabu bingwa Afrika. 

"Hakuna taarifa iliyotoka kwamba anaweza kuanza kucheza, taarifa iliyotoka ni Kamusoko kupona majeraha, mchezaji akitoka kwenye majeraha hawezi kuanza kucheza mechi za ushindani moja kwa moja, anaanza kufanya mazoezi taratibu hadi awe kwenye kiwango cha asilimia 100 cha utimamu wa mwili ili aweze kupambana", amesema Dismas.

Pamoja na hayo, Dismas ameendelea kwa kusema "anaweza akapona leo kesho akachezeshwa mechi akaumia tena, kwa hiyo Kamusoko alipewa muda, daktari amerejea atamfanyia uchunguzi ili kuthibitisha kama tayari anaweza kurejea uwanjani kwa ajili ya mechi".

Kwa upande mwingine, timu ya Yanga itashuka dimbani leo mjini Songea kuivaa Majimaji FC katika mashindano ya Kombe la Shirikisho