Jumanne , 4th Jun , 2019

Shirikisho la Soka Tanzania TFF limetangaz kuwa klabu ya Yanga itaungana na Simba kushiriki michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika msimu ujao.

Yanga

TFF imesema kuwa taarifa hiyo imethibitishwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF, ambapo katika michuano ya shirikisho barani Afrika, Azam FC na KMC zitaiwakilisha Tanzania.

Hiyo ni kutokana na Tanzania kupanda katika viwango vya ubora wa vilabu katika miaka ya karibuni ambapo hivi sasa imekuwa katika nafasi ya 12, ambapo itapata nafasi ya kuwakilisha timu 4 katika michuano ya kimataifa.

Isome barua ya TFF hapo chini.