Yanga yatoa sababu 4 za kutoshiriki Kimataifa

Jumapili , 9th Jun , 2019

Klabu ya soka ya Yanga imeweka wazi kuwa haitashiriki michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Kagame, kwa mwaka 2019.

Yanga SC

Yanga imejitoa kwenye michuano siku chache baada ya wapinzani wao Simba kufanya hivyo huku wao wakieleza sababu zao 4.

Kwa mujibu wa taarifa ya Yanga sababu hizo ni wachezaji kumaliza mikataba na kutokamilika kwa baadhi taratibu za usajili wa wachezaji wapya.

Sababu nyingine ni kuwa Kocha wao mkuu Mwinyi Zahera na wachezaji kuwa michuano ya AFCON 2019 nchini Misri. Pamoja na wachezaji waliobaki kuruhusiwa kwenda mapumzikoni.

Yanga ni mabingwa mara 5 wa kombe hilo ambalo walichukua katika miaka ya 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012.