Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele akiwatoka wachezaji wa Mtibwa Sugar
Mabao ya Yanga katika ushindi wa mabao 2-0 yamefungwa na Saido Ntibanzokiza aliyefunga bao la kwanza katika dakika za nyongeza kipindi cha kwanza na Fiston Mayele aliifungia timu ya wananchi bao la pili dakika ya 66.
Bao alilofunga Mayele ni bao lake la 7 msimu huu kwenye Ligi akiwa anashika nafasi ya pili ikiwa ni idadi sawa na George Mpole wa Geita Gold mwenye mabao 7 pia kwenye orodha ya wafungaji wakiwa nyuma ya Kinara Realint Lusajo wa Namungo FC mwenye mabao 10.
Ni kwa mara ya 3 mfululizo Mtibwa Sugar wanafungwa na Yanga kwenye michezo ya ligi Kuu kwani msimu uliopita walifungwa michezo yote miwili ya Lgi ambapo Yanga walishinda michezo yote kwa ushindi wa bao 1-0.
Kwa ushindi huu Yanga wamefikisha alama 39 na wanaongoza Ligi kwa tofauti ya alama 8 dhidi ya watani zao wa jadi Simba SC ambao wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 3 wote wakiwa wamecheza michezo sawa michezo 15. Na mtibwa Sugar wamesalia na alama zao 12na wanasalia nafasi ya 15 kwenye msimamo.






