Zahera ang'oka Yanga, fahamu kuhusu malipo yake

Jumanne , 5th Nov , 2019

Mwenyekiti wa Yanga Dkt. Mshindo Msolla, amethibitisha klabu hiyo kuvunja benchi lake lote la ufundi na kuanza upya.

Sehemu ya benchi la ufundi la Yanga

Amesema wamefikia uamuzi huo kutokana na mwenendo wa klabu hiyo kwenye mashindano mbalimbali waliyoshiriki msimu huu, ikiwemo Ligi kuu, Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.

Akiongea na wanahabari leo Novemba 5, 2019 Makao makuu ya klabu hiyo Msolla amesema wamemalizana salama na watu wote wa kwenye benchi la ufundi.

'Tumevunja benchi lote la ufundi mpaka mlinzi, na tunaanza upya, kwasasa tunamalizia tu taratibu za kuagana na kama wengine wataendelea basi watapitia utaratibu mpya', amesema Msolla.
Zaidi Tazama Video hapo chini