Ijumaa , 10th Jul , 2020

Zlatan Ibrahimovic amesema huenda akaondoka kwenye klabu yake ya AC Milan mwishoni mwa msimu huu, endapo mambo hayatobadilika kwenye klabu hiyo.

Zlatan Ibrahimovic (pichani) katika mchezo wa Serie A dhidi ya Inter Milan.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa vilabu vya Manchester United, PSG na Barcelona, alirejea Milan kama mchezaji huru Januari mwaka huu, lakini haelewani na mtendaji mkuu wa Mila Ivan Gazidi juu ya mwelekeo wa timu hiyo kwenye Serie A.

''Ibra alizaliwa kucheza mpira na bado ni bora katika kucheza mpira,Tutaona jinsi ninavyohisi katika miezi mwili,Tutaona pia kitakachotokea na kilabu.Ikiwa hali ndio hii, kuwa mkweli, kuna uwezekano nisionekane Milan msimu ujao.

Milan ipo nafasi ya 7 kwenye ligi ya Italia maarufu kama serie A, ikiwa pungufu alama 2 kuzifikia Roma na Napoli, ili kupata nafasi ya kushiriki Europa League msimu ujao, michuano ambayo kwa Zlatan amesema hayana hadhi yeye kucheza.

"Ibra siyo mchezaji wa Europa League na Milan siyo klabu ya Europa League."

Hali bado haieleweki ndani ya Milan kwenye benchi la ufundi, huku kukiwa na mipango ya kumwondoa kocha Stefano Pioli na nafasi yake akitajwa kocha wa zamani wa RB Lepzig ya Ujerumani Ralf Rangnick.

Ikumbukwe nyota huyo wa kimataifa wa Sweden alikua na mchango mkubwa wakati AC Milan inainyuka Juventus bao 4-2,na hata baada ya mechi hiyo alitamka kwamba iwapo angesajiliwa mwanzoni mwa msimu , angeisaidia Rossoneri kutwaa Scudetto.