Jumatatu , 4th Jul , 2022

uongozi wa Klabu ya Azam FC imefanikiwa kuishinda vita ya kuipata saini ya mshambuliaji Abdul Seleman ‘Sopu’ ambaye alikuwa anawindwa na vigogo Simba na Yanga.

Mshambuliaji mpya wa Azam Fc Abdul Seleman ‘Sopu’

Dakika chache zilizopita Azam imemtambulisha rasmi nyota huyo aliyewahi kuichezea Simba na kumpa mkataba wa miaka mitatu akitokea Coastal Union.

Sopu ameingia midomoni mwa wadau wa soka nchini baada ya kuwa katika kiwango kikubwa msimu ambapo kwenye Ligi Kuu amemaliza na mabao nane huku katika kombe la FA amemaliza akiwa mfungaji bora wa mashindano hayo kwa kumaliza na mabao tisa huku kwenye mchezo wa fainali akipiga  'Hat-trick'.

Azam wanaonekana kuwa jambo lao msimu ujao ambapo hadi sasa tayari wameshakamilisha na kuwatambulisha wachezaji wanne ambao ni Tape Edinho, Kipre Junior, Isah Ndala, Cleophas Mkandala pamoja na Abdul Seleiman.