Jumatatu , 5th Dec , 2022

Mchezo wa dhidi ya Coastal Union uliopigwa Desemba 2, katika Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga tulioibuka na ushindi wa mabao 3-0 ulikuwa wa 15 ambao umekamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi.

Mpaka tumekamilisha mzunguko wa kwanza tumefanikiwa kukusanya alama 34 tukicheza mechi 15 tukishinda 10 sare nne na kupoteza moja.

Tumefanikiwa kufunga mabao 31 na kuruhusu kufungwa saba pekee tukiwa na uwiano wa mabao 24.

Nyota wetu 11 kwa pamoja ndiyo waliofunga idadi hiyo ya mabao huku Moses Phiri akiwa kinara akicheka na nyavu mara 10.

Wachezaji waliofunga katika mzunguko wa kwanza wa ligi

1. Moses Phiri 10
2. John Bocco 4
3. Augustine Okrah 3
4. Pape Sakho 3
5. Habib Kyombo 2
6. Mzamiru Yassin 2
7. Clatous Chama 2
8. Dejan Georgijevic 1
9. Jonas Mkude 1
10. Peter Banda 1
11. Shomari Kapombe 1

Wachezaji waliotoa assist kwenye mzunguko wa kwanza

1. Clatous Chama 7
2. Mohamed Hussein 4
3. Moses Phiri 2
4. Mzamiru Yassin 2
5. Mohamed Ouattara 1
6. Kibu Denis 1
7. Augustine Okrah 1
8. Gadiel Michael 1
9. Shomari Kapombe 1
10. Jonas Mkude 1
11. Sadio Kanoute 1

Mlinda Aishi Manula amepata Clean Sheet 9 na ndiye kinara akiongoza makipa wote wa Ligi Kuu ya NBC.