
Magoli ya Yanga SC yamefungwa na kiungo wake mshambuliaji Stephan Aziz Ki dakika 64 na la pili limefungwa na winga Bernard Morrison dakika 90+2 ambaye alitokea benchi kuchukua nafasi ya winga Tuisila Kisinda.
Ushindi huo unawapa faida Yanga SC kuichungulia fainali ya michuano hiyo kuelekea mchezo wao wa marudiano dhidi ya Marumo Gallants unaotaraji kuchezwa Mei 17, 2023 nchini Afrika Kusini ambapo ili Marumo ifuzu fainali inahitaji kushindi utofauti wa magoli 3.