Jumatatu , 15th Feb , 2016

Msanii Bebe Cool ambaye anampigia kampeni mgombea urais kwa awamu nyingine ambaye pia ni Rais wa sasa wa nchini Uganda Yoweri Kaguta Museven, amesema atatumia uwezo wake kuwapeleka watu sehemu sahihi.

Bebe Cool ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) na kusema kuwa ameshazunguka karibia nchi nzima akifanya maonesho, hivyo anajua jinsi nchi ilivyokuwa miaka 20 nyuma na sasa hivi, hivyo atatumia uwezo wake kufanya hivyo kuwahamasisha watu kwenda sehemu sahihi.

“Mimi ni mtu sahihi kuwambia nchi iko vipi, nimefanya maonesho kila wiki kwa miaka 20 iliyopita, naijua tofauti ya kila kijiji miaka 15 – 20 iliyopita na sasa, kwa hiyo kama ni kuwaongoza watu wangu kwenye sehemu sahihi, nafikiri kwa kutumia uwezo wangu na wasifu wangu, nitaitumia kwa sababu iliyo sahihi”, alisema Bebe Cool.

Bebe Cool amekuwa miongoni mwa wasanii wakubwa wanaoongoza kampeni za urais za Rais Museven nchini Uganda, akiwemo pia Jose Chameleone, Juliana Kanyomozi, Weasel na Radio, na Irene Namubiru, ambapo uchaguzi wake unatarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi huu.