Jumatano , 16th Mar , 2016

Wakati makundi mengi ya muziki yaliyovuma nchini miaka ya nyuma yakishindwa kurudi kwenye game la muziki licha ya kuwa ni kiu ya watu wengi kuwaona wasanii wa zamazi wakirudi kwenye game, msanii Makamua ameamua kurudishwa kwenye game.

Master Jay

Makamua ni moja ya 'Member' waliounda kundi la Wakali Kwanza lililokuwa chini ya MJ Records na kwa taarifa ambazo E-News imezipata kutoka kwa Makamua ni ujio mpya wa kundi hilo ambalo linaundwa na Makamua, Q JAY na Joselin likiwa chini ya MJ.

Q Jay alishawahi kuapa kuwa hatofanya tena muziki ya kidunia na kufanya nyimbo zinazo mpendeza Mungu kwa maana ya nyimbo za injili za kumtukuza Mungu lakini sasa ameonekana kurejea tena kule alikodai kuwa ametoka.