
Maandamano katika miji mbalimbali nchini Marekani
Wengi walikuwa wakipaza sauti na kusema 'Sio Rais Wangu' huku wengine wakichoma moto picha za Bw. Trump.
Maandamano hayo yamefanyika jijini New York mbele ya jengo la Trump Tower ambapo watu 15 wamekamatwa.
Maandamano mengine yameshuhudiwa Oakland California, Chicago, Portland Oregon , Boston, Seattle, Philadelphia , San Fransisco na Washington DC ambapo watu waliwasha mishumaa kuashiria huzuni.
Bw. Trump anakuwa Rais wa 45 wa Marekani baada ya kupata ushindi uliowashangaza wengi dhidi ya Bi Hillary Clinton wa chama cha Democratic .
Rais huyo mteule baadaye alikutana na Rais Barack Obama Ikulu ya White House na kufanya mazungumzo yenye lengo la kuhakikisha mabadiliko ya uongozi yanafanyika kwa utaratibu ulio sahihi huku akiahidi ushirikiano.
Rais Obama ambaye alimuelezea Bw. Trump kama mtu asiyefaa kuongoza , ametoa wito kwa Wamarekani wote kukubali matokeo na kumuunga mkono katika kuliunganisha taifa hilo lenye nguvu duniani.