Jumanne , 6th Dec , 2016

Serikali inatarajia kuanzisha tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii (blogs) nchini kuanzia mwaka 2017.

Wazir Nape Nnauye akizungumza na Tanzania Bloggers Network (TBN)

 

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini.

Waziri Nape amesema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.

Aidha, Waziri Nape amesema kuwa tayari serikali imeanza mazungumzo na makampuni na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kudhamini tuzo hizo ili kuhakikisha kuwa washindi wanapatikana kwa uwazi.

“Tuzo hizo zitakuwa za kwanza kwa namna zitakazovyoendeshwa kwa uwazi hivyo makampuni zaidi yanakaribishwa kuweza kuzidhamini mashindano hayo yatakayojielekeza kwenye nyanja tofauti” alisema Waziri Nape.