Jumatatu , 19th Mei , 2014

Kamati ya uchaguzi ya simba hii leo imetangaza orodha ya awali ya wagombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya klabu hiyo katika uchaguzi ambao utafanyika june 29 mwaka huu.

Dkt Damas Ndumbaro, Mwenyekiti kamati ya uchaguzi Simba

Kamati ya uchaguzi ya simba hii leo imetangaza orodha ya awali ya wagombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya klabu hiyo katika uchaguzi ambao utafanyika june 29 mwaka huu.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Dr. Damas Ndumbaro amesema wagombea wote 41 katika nafasi mbalimbali wamepitishwa kwa kuwa wamekidhi matakwa ya ujazaji fomu za ugombea.

kwa upande mwingine mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Simba Dr. Damas Ndumbalo amesema zoezi la kupokea pingamizi linaanza rasmi hapo kesho na kumalizika Alhamisi may 22 mwaka huu.

Aidha Ndumbaro amesema mwenye haki ya kuleta pingamizi ni mwanachama wa Simba na anapaswa kuja na vithibitisho vya hoja ya pingamizi,akiandika jina kamili, anwani yake na namba ya simu ya mkononi.

Wakati huo huo kamati ya utendaji ya klabu ya simba imefanya mabadiliko katika kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo kwa kufuata kanuni za uchaguzi wa TFF.

Katibu mkuu wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga amesema kwa kuwa timu hiyo haina kanuni za uchaguzi ndiyo maana wamelazimika kutumia kanuni za TFF na hivyo sasa idadi ya wajumbe wanatakiwa wawe watano badala ya saba walionao sasa huku nafasi za mwenyekiti na makamu wa kamati ni lazima wawe wanasheria