
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo amesema mbali na watu 17 kushikiliwa na polisi pia ofisi yake imepokea majina zaidi ya 20 ya watu wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya.
Amesema, Rais Dkt. John Magufuli, ametangaza kwamba, hiyo ni vita ya nchi nzima, na kwamba, baada ya wananchi kusikia vita ya dawa za kulevya ikiendelea mkoani Dar es salaam,wameamua kuleta majina zaidi ya 20 ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya, wakisema wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali kupiga vita dawa za kulevya .
Amesema ,kamati ya ulinzi na usalama imeunda kikosi kazi cha kushughulikia majina yanayoletwa ili kubaini kama ni kweli wanajihusisha na dawa za kulevya.