Jumatano , 5th Apr , 2017

Muigizaji na kada wa CHADEMA, Wema Sepetu  amemtaka msanii asiyekaukiwa matukio mitandaoni Harmorapa kuacha mara moja kumtumia kama ngazi katika  kutafuta riziki zake bali amuheshimu kama dada na msanii mwenzake.

Harmorapa na Wema Sepetu

Wema amecharuka katika mtandao wake wa instagram  leo ikiwa ni siku chache zimepita tangu msanii huyo anayetamba na ngoma ya 'Kiboko ya mabishoo' kutangaza kuwa anampenda msanii huyo na kwamba anaumizwa na jinsi watu wanavyomuumiza kimapenzi.

Aidha mwanadada huyo amemtaka msanii huyo kupigana jinsi atakavyoweza kulifikisha jina na muziki wake juu pasipo kumtumia yeye kama njia na kuongeza ni kumvunjia heshima mbele ya familia, chama, marafiki pamoja na mpenzi aliyenaye.

"Sijawahi kumchukia yeyote anayehangaika kutafuta riziki yake kwa kuwa nami pia natafuta. Ila mdogo wangu Harmorappa u are getting too much. Pigana na namna utakavyo kupeleka muziki na jina lako juu but get me out of this. Nakuheshimu kama msanii mwenzangu lakini hili la kunadi kunitaka kimapenzi na kuonyesha utayari wa kufanya mambo kadha wa kadhaa kwangu please waambie wengine unaodhani mnawezana ila mimi siyo wa aina hiyo". aliandika Wema.

Katika kuonesha kuwa muigizaji huyo amekerwa na kauli ya Harmorapa, ameongeza kwamba  "Do u think na mimi ni wa aina hiyo? Usinidharaulishe.... Nadhani kuna busara ya wewe to look for another one butan not for you and i hope utanipa heshima yangu kama dadaako, msanii mwenzako lets stop there"